array(0) { } Radio Maisha | Waziri Macharia atakiwa kung'atuka

Waziri Macharia atakiwa kung'atuka

Waziri Macharia atakiwa kung'atuka

Na Rosa Agutu,

NAIROBI, KENYA, Shinikizo linaendelea kutolewa kwa Waziri wa Uchukuzi, James Macharia kung'atuka mamlakani kufuatia agizo la serikali kwamba makasha ya mizigo yasafirishwe kupitia Reli ya Kisasa, SGR.

Akihutubu wakati wa maandamano ya kila Jumatatu maarufu  Okoa Mombasa, Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amesema uchumi wa Pwani unazidi kudorora kufuatia agizo hilo.

Amesisitiza kwamba wataendelea kushiriki maandamano hadi pale serikali itakapositisha usafirishaji wa mizigo kupitia SGR.

Amesema zaidi ya vijana elfu ishirini wamepoteza ajira katika Kaunti ya Mombasa, hali inayosababisha kupanda kwa gharama ya maisha.