array(0) { } Radio Maisha | Sonko aahidi kuendelea kuwakabili wanyakuzi wa ardhi

Sonko aahidi kuendelea kuwakabili wanyakuzi wa ardhi

Sonko aahidi kuendelea kuwakabili wanyakuzi wa ardhi

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema ataendelea kuwakabili wanaonyakua ardhi za umma jijini Nairobi.

Akizungumza muda Jumatatu katika mahojiano ya kipekee katika kipindi cha Maisha Asubuhi -Radio Maisha, Sonko amesema masaibu yanayomwandama yanasababishwa na juhudi zake za kuwakabili watu wanaoendeleza unyakuzi wa ardhi vilevile juhudi zake katika kuukabili ufisadi nchini.

Akirejelea kisa cha kuporomoka kwa jengo la Shule Binafsi ya Precious Talent, Sonko amesema ameendelea kukosolewa kwa kuwasimamisha kazi maafisa wanaohusika katika kisa hicho, akisema hajawahi kuwafuta kazi maafisa wake serikalini na badala yake huwasimamisha kazi ili kufanikisha uchunguzi.

Wakati uo huo, amemkosoa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Nairobi, Abdi Guyo akidai kuwa amekuwa akimtishia katika juhudi zake za kuwakabili maafisa fisadi.

Aidha, amesisitiza kwamba sehemu ambayo jumba la EACC lilijengwa ni ardhi ya umma na kwamba hawakufuata sheria katika ujenzi wa jumba hilo, akisisitiza kwamba atafanikiwa katika vita dhidi ya ufisadi.