array(0) { } Radio Maisha | Shughuli ya kuitafuta miili Pokot Magharibi kuendelea
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli ya kuitafuta miili Pokot Magharibi kuendelea

Shughuli ya kuitafuta miili Pokot Magharibi kuendelea

Na Sam Amani,

NAIROBI, KENYA, Shughuli ya kuitafuta mili iliyofukiwa ardhini kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi inatarajiwa kuendelea Jumatatu kwa siku ya tatu, tangu kutokea kwa mkasa wa maporomoko ya ardhi, kusini mwa kaunti hiyo.

Aidha, idadi ya watu waliofariki kufikia jana jioni ilikuwa hamsini na mmoja. Akitoa ripoti hiyo Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo alisema kuwa watu elfu kumi wameachwa bila makao huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Maafisa wa Jeshi la Ulinzi KDF, Idara ya Polisi, Shirika la Msalaba Mwekundu vilevile maafisa wa Kitengo cha Kukabili Majanga wataendeleza shughuli hiyo huku wakitoa msaada na ushauri nasaha kwa familia zilizoathirika. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa mkasa huo kuwa tukio la kipekee kwa kuwa hawajawahi kushuhudia tukio hilo. Aidha wamesema kuwa iwapo mvua itaendelea kunyesha huenda ikatatiza shughuli ya uopoaji.

Hata hivyo, Lonyangapuo ametoa orodha ya maeneo ambapo wakazi hao wanaweza kuyatembelea ili kupata usaidizi wowote kuhusiana na mkasa huo.

Maneo hayo ni; Ofisi ya Kuanti ndogo iliyoko Makutano na Giro. Ofisi inayoshughulika na utoaji misaada iliyo katika makao makuu ya ofisi ya Gavana, ofisi ya Usimamizi wa Hospitali ya Kapenguria, ofisi za Kuu za Wadi za Tapach, Weiwei na Batei pamoja na ofisi ya mipango ya kaunti iliyoko katika jumba la CVS plaza jijini Nairobi.

Gavana huyo ameongeza kuwa wanafanya kila juhudi kutafuta nambari itakayowawezesha wananchi kutoa mchango wa kifedha yaani PAY BILL kufikia Jumatatu kwa ajili ya waathiriwa.

Hayo yakijiri, Serikali ya Kaunti jirani ya Trans-Nzoia ilithibitisha kupokea ombi kutoka Hospitali ya Kapenguria ikiomba kusaidiwa kuhifadhi mili ikisema Hifadhi ya Kapenguria haina uwezo wa kuishughulikia mili hiyo yote.