array(0) { } Radio Maisha | KPL ni tofauti na NSL, Wazito FC watapata taabu sana
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

KPL ni tofauti na NSL, Wazito FC watapata taabu sana

KPL ni tofauti na NSL, Wazito FC watapata taabu sana

Mashabiki wa mchezo wa kandanda nchini wameikashifu vikali Wazito fc na kuilaani timu hiyo huku wakiongezea kwamba mibabe hao wa hela hawatapata ufanisi ligii kuu nchini KPL.

Mapema jumapili jijini Nairobi, katika uwanja wa Camp toyoyo, mashabiki hao walionesha masikitiko na timu hiyo.

“KPL ni ligii tofauti sana na kule walikotoka NSL. Msimu jana sikufurahishwa na vile walivyopandishwa ligii kuu. Kuna baadhi ya mechi zao ungeona tu wazi wazi waamuzi walikuwa wanaegemea upande mmjoa. Nafikiria haya mambo ambayo walikuwa wameyazoea bado yanawasumbua, maanake sasa kule KPL utamhonga nani,” aliuliza kwa kejeli Fanuel, shabiki sugu wa Afc leopards kutoka mtaani Babadogo.

Msimu jana Wazito fc walipokuwa wakishiriki katika ligi ya daraja la pili nchini NSL, tetesi za upangaji wa mechi na ufisadi kwa ujumla ziliongezwa sauti. Baadhi ya vilabu kama vile Modern Coast fc, Kibera Black Stars na wengine walilamika sana kuhusu maamuzi ambayo yaliegemea upande mmoja haswa katika mechi dhidi ya Wazito fc.

“ Hakuna ufisadi wowote unawo endelea, timu zote mbili huajibika kuwalipa waamuzi. Kwa hivyo wale ambao wana lalamika ya kwamba tunawahonga waamuzi huenda wana chuki binafsi,” alisema msimu jana Solomon Alubale, mwenyekiti wa klabu hiyo katika mahojiano spesheli na meza ya michezo Redio Maisha.

Wazito fc ambao kwa sasa wanamilikiwa na bwanyenye mwarabu Ricardo Badoer, walirejea katika KPL msimu huu kwa fujo na kishindo. Waliwasajili wachezaji nyota kama vile akina Elvis Rupia, Hassan Ali Abondo, Karim Nzyigimana, Abuba Sibomana kuwataja tu lakini kwa uchache.

“ Timu si majina lakini ukufunzi na pia kuajibika kwa haki. Ona sisi timu yetu Gormahia, ndio Pollack aliwapata wachezaji wengi wageni msimu huu, lakini si walikuwa niwa kawaida tu KPL ina wenyewe, tena huko hakuna kula rahisi, lazima utoe kijasho,” alikejeli pia Oti, shabiki wa Gormahia kutoka mtaa wa Hamza Makadara, Nairobi.

Msimu jana kulikuwa na tetesi ya kwamba vilabu ambavyo vilishiriki NSL na vilikuwa na ubabe wa hela, vilihusika pakubwa na upangaji wa mechi. Ligii hiyo ya NSL haikuwa na mdhamini wa waamuzi wala kupata hela zozote kutoka kwa shirikisho la kandanda FKF, jambo ambalo mibabe wa hela walilitumia kwa mafao yao.

Wazito fc kwa sasa imewafuta kazi makocha wawili chini ya takriban miezi miwili tangu msimu uanze. Mmiliki wa klabu hiyo pia maajuzi amewatishia wachezaji wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter ya kwamba atawafuta kazi iwapo hawataonesha mchezo mzuri na kupata matokeo bora. Kwa sasa wanafunzwa na muingereza Stewart Hall, mkufunzi wa tatu tangu msimu huu uanze.