array(0) { } Radio Maisha | Sitatia saini hadi nihakikishiwe Pep, atasalia Man City
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sitatia saini hadi nihakikishiwe Pep, atasalia Man City

Sitatia saini hadi nihakikishiwe Pep, atasalia Man City

Kiungo mshambulizi wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Manchester City Raheem Sterling amekataa kuzidisha mkataba hadi klabu hiyo imuhakikishie Josep Guardiola ataendelea kuwa mkufunzi.

Sterling anatazamiwa kulipwa  kitita cha pauni elfu 450 kila wiki kwa mkataba huo mpya, lakini kiungo huyo mzawa wa jiji la Kingston, Jamaica miaka 24 iliyopita, amesema aka.

Kiungo huyo ambaye pia ni naibu nahodha katika timu ya taifa ya Uingereza, amekuwa na uswahiba mkuu na Guardiola. Penyenye za sema kwamba Guardiola ambaye mkataba wake na Man city utakamilika baada ya miezi 18 huenda akaihamia kwingine.

“ Tangu ujio wangu katika ligii kuu ya Uigereza, nimefurahia sana changamoto za wachezaji na wakufunzi walio bora. Ona sasa Jose Mourinho amerejea na Spurs, ina maanisha kwamba ushindani uliopo niwa hali ya juu. Lengo langu sasa nikujaribu kushinda klabu bingwa barani ulaya na Man City, sioni haja ya kwenda kwingine,” alikiri Josep Guardiola mapema wiki hii siku ya jumatatu.

Sterling aliondoka Liverpool na kujiunga na Man City msimu wa 2015/2016. Baada ya Manuel Pellegrini kuondoka, Guardiola alimhakikishia kwamba siku zote atasalia katika mipango zake na kumwahidi watashinda mataji pamoja.

Kiungo huyo maajuzi alipapurana na Joe Gomez katika mechi yao dhidi ya Liverpool fc, jambo ambalo pia lilimsababishia balaa katika timu ya taifa. Katika wakati huo mgumu, Guardiola ndiye wa pekee aliyemjali na kumpa moyo.

Sterling kwa sasa analipwa pauni elfu 300 kwa wiki na iwapo basi atahakikishiwa kwamba mkufunzi wake Guardiola atasalia Man City, anataongezwa elfu 150 zingine ambazo zitamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi katika ligii kuu ya Uingereza.