array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya waliofariki dunia kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi Kaunti ya Pokot Magharibi imefikia 51; 10,000 wameachwa bila makao
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya waliofariki dunia kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi Kaunti ya Pokot Magharibi imefikia 51; 10,000 wameachwa bila makao

Idadi ya waliofariki dunia kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi Kaunti ya Pokot Magharibi imefikia 51; 10,000 wameachwa bila makao

Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi imefikia hamsini na mmoja. Amesema gavana wa Kaunti hiyo John Lonyangapuo. Lonyangapuo aidha amesema kwmaba watu elfu kumi wameachwa bila makao, huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Hadi sasa maafisa wa serikali wakiongozwa na Jeshi la Ulinzi KDF , Idara ya Polisi, Shirika la Msalaba Mwekundu na Kitengo cha kukabili majanga, wanaendele kutoa msaada kwa walioathirika. Majeruhi wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Kapenguria, huku maafisa mbalimbali wakitumwa kupeleka chakula cha msaada na wengine kutoa ushauri nasaha.

Lonyangapuo ametoa orodha ya maeneo matano ambapo wakazi hao wanaweza kuyatembelea ili kupata usaidizi wowote.

Maneo hayo ni

  • Ofisi ya Kuanti ndogo iliyoko Makutano na Giro.
  • Ofisi inayoshughulika na utoaji misaada iliyo katika makao makuu ya ofisi ya Gavana
  • Ofisi ya Usimamizi wa Hospitali ya Kapengutia.
  • Ofisi za Kuu za Wadi za Tapach, Weiwei na Batei

Pamoja na

  • Ofisi ya mipango ya kaunti iliyoko katika jumba la CVS Plaza iliyo hapa Nairobi.

Gavana Lonyangapuo ameongeza kuwa wanafanya kila juhudi kutafuta nambari itakayowawezesha wananchi kutoa mchango wao yaani  PAY BILL kufikia kesho.