array(0) { } Radio Maisha | Eliud Kipchoge ndiye mshindi wa mwanariadha bora wa tuzo ya IAAF, 2019

Eliud Kipchoge ndiye mshindi wa mwanariadha bora wa tuzo ya IAAF, 2019

Eliud Kipchoge ndiye mshindi wa mwanariadha bora wa tuzo ya IAAF, 2019

Mshikilizi wa rekodi ya mbio za marathon Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda tuzo ya mwanariadha bora wa IAAF ya mwaka 2019 katika hafla iliyoandaliwa Monaco.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Kipchoge amesema amefurahishwa zaidi na kuvunja rekodi ya mbio za marathon kwa kutumia saa 2 na dakika moja vilevile saa moja na dakika hamsini na tisa. 

Kipchoge aliweka rekodi mpya ya mbio za marathon jijini Berlin mwezi Septemba mwaka uliopita kwa kuvunja rekodi iliyowekwa hapo awali na sekunde 78.

Aidha, Kipchogealiandiskisha historia kwa kuwa mwanadamu wa kwanza mwaka huu kwa kukimbia marathon kwa kutumia muda wa saa moja na dakika hamsini na tisa maarufu INEOS Marathon, zilizofanyika jijini Vienna Austria.

Kipchoge amewapiku Joshua Cheptegei raia wa Uganda na ambaye ni bungwa wa mbio za dunia za mita 200 na Noah Lyles USA.

Dalilah Muhammad wa Marekani ameibuka mshindi wa mwanariadha bora duniani katika kitengo cha wanawake, na kumshinda  Brigid Kosgei, wa Kenya,  Shelly Ann Fraser  wa Jammaica na  Sifa Hassan wa Uholanzi.