array(0) { } Radio Maisha | Nyota wa Chelsea matatani na Lampard
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Nyota wa Chelsea matatani na Lampard

Nyota wa Chelsea matatani na Lampard

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Chelsea fc Ross Barkley yumo tena matatani na mkufunzi wake Frank Lampard.

Haya yanajiri baada ya likizo fupi ya michuano ya kimataifa baina ya mataifa tofauti tofauti. Wakati huo ligii za barani ulaya zilikuwa zimesimashiwa na Ross Barkley aliomba ruhusa kutoka kwa timu yake Chelsea fc, akaenda zake Dubai kupunga unyunyu.

Kumbe unyunyu huu ulikuwa ni chovya chovya za buyu la asali katika vilabu vya anasa jijini Dubai. Barkley mwenye umri wa miaka 25 amekuwa nje kwa tabriban mwezi mmoja sasa baada ya kujeruhiwa kisigino mapema.

Ikumbukwe ya kwamba mwezi wa Septemba nyota huyo alipapurana na dereva wa taxi jijini Liverpool baada ya kukata kulipa na kumwaga mwaga  vibanzi garini.

“Ni kweli vijana walikuwa na siku moja ya mapumzisho, lakini nilitumahi watapumzika wala sikwenda vilabuni kulewa. Barkley ni kijana mchapa kazi na mwenye bidii, lakini swala la nidhamu ni muhimu sana kaika taaluma hii. Lazima uwe kigezo kwa kizazi ibuka. Sitakubali tabia kama hii.” Alinukuliwa akisema Frank Lampard baada ya tukio hilo la mwezi Septemba.

Barkley tayari amesha anza mazoezi na hata maajuzi Gareth Southgate alimjumuisha katika kikosi cha timu ya taifa japo alijiondoa tena. Sasa macho yote yanamwangalia Frank Lampard haswa baada ya kutoa sheria kali kambini maajuzi. Tukio hili la Barkley lina jiri pia wakati Chelsea inajiandaa kuvurugana na Manchester City leo jioni ugenini Eitihad.