array(0) { } Radio Maisha | Bandari itabeba ligi kabla ya Ingwe; Muhdin
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Bandari itabeba ligi kabla ya Ingwe; Muhdin

Bandari itabeba ligi kabla ya Ingwe; Muhdin

Mkurugenzi wa michezo katika Klabu ya Bandari fc Twahir Muhdin amezua hisia mseto kwa mashabiki alipo tangaza ya kwamba klabu yake Bandari fc itashinda ligii kuu nchini KPL kabla ya mabingwa mara 13 Afc leopards.

Akizungumza na Redio Maisha dawati la michezo mapema jumamosi, Muhdin alionesha ujasiri.

“Kizuri na cha muhimu ni kwamba Bandari fc ni timu ambayo imejipanga. Tuna miundo misingi na ubabe wa hela ukilinganisha na Ingwe. Lengo letu ni kushinda ligi sasa. Tuseme kama misimu miwili ijayo, tutatimizia lengo letu. Ili kuwa mabingwa lazima tuwang’atue Gormahia kutoka kileleni. Nina uhakika ya kwamba tutatimiza haya kabla ya Afc leopards, siku hizi hawana upinzani kama vile zamani.” Alisema mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya taifa Harambee Stars ambaye pia aliwahi kuihudumia Afc leopards akiwa katika kamati ya kiufundi msimu wa 2008/2009.

Mapema siku ya alhamisi wiki hii, vijana hao ambao wanafunzwa na  Bernard Mwalala walitoka saree ya mabao mawili kwa mawili na hio Afc leopards wakiwa nyumbani Mbaraki. Ilikuwa mechi ambayo kwamba wengi wahakiki wa kandanda nchini wali ipigia upato Bandari kushinda nyumbani lakini mambo yaka waendea ubaya.

“Vijana wangu wanakosa motisha na nidhamu. Mechi kama hii ilikuwa rahisi sana kwetu kupata ushindi. Ilikuwaje Bandari wakatoka nyuma mara mbili na kupata saree Hapa tumefika sasa ni Mungu tu.” aliuliza kwa ghadhabu Andre Cassa Mbungo mkufunzi wa Ingwe baada ya mechi hiyo dhidi ya Bandari.

Bandari Fc, timu yake Twahir Muhdin kwa sasa wanashikilia nafasi ya 12 baada ya mechi tisa na alama 12. Afc leopards nawo wako katika nafasi ya nane, baada ya mechi kumi wana alama 16.

“ Kila kitu ni pole pole. Ni kweli kwamba msimu huu tume anza vibaya katika KPL, lakini tuta boreka. Nafikiria safari yetu katika michuano ya barani Afrika pia imetufunza mengi. Vijana wetu sasa wamerejea nchini na fikira zao zote sasa zimerejea katika KPL. Tuta makinika, mashabiki wetu wasife moyo,” alisema kwa matumaini Twahir Muhdin.

Bandari fc ambao walishinda taji la ngao nchini msimu jana. Wameshiriki katika michuano ya kombe la mashirikisho barani Afrika msimu huu na kupiga hatua ya kupigiwa mfano. 

Lengo lao sasa ni kutwaa ubingwa na KPL na kuwang’atua Gormahia kileleni kabla ya Afc leopards kuwazia hilo. Kwa mashabiki wa Bandari fc ni subira tu sasa ambayo wana imani itavuta heri siku moja, kwa wana Ingwe ni jitihada za msafiri ambaye tayari yuko bandarini, wana imani watafika kabla ya Bandari fc.

Kila mwamba ngoma huivutia kwake, kutoka kwetu Redio Maisha ni kuwatakia  heri za fanaka tu, kwa mibabe hawa wawili wa soka nchini Kenya.