array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya waliofariki Pokot Magharibi kufuatia maporomoko imefikia, 24

Idadi ya waliofariki Pokot Magharibi kufuatia maporomoko imefikia, 24

Idadi ya waliofariki Pokot Magharibi kufuatia maporomoko imefikia, 24

Watu24 wanahofiwa kufariki dunia baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kufuatia maporomoko ya ardhi katika Kaunti ya Pokot Magharibi.

Chifu wa Nyarkulian, Joel Bulal amesema watu kumi na wawili walifukiwa na mchanga usiku wa kuamkia leo huku watu wengine wanne wakifukiwa katika Kijiji cha Parua. Vijiji Vingien ambavyo vimeathirika ni  Tamkal, Weiwei, Parua na Tapach.

Wakari uo huo usafiri umetatizika baada ya daraja ambazo ni Weiwei na Ortum kusombwa.

Bulal amesema shughuli za uokoaji zinaendelea kwa sasa. Aidha Shirika la Msalaba Mwekundu tayari limethibitisha kwamba maafisa wake wamefika katika maeneo hayo ili kusaidia katika shughuli ya uokoaji.