array(0) { } Radio Maisha | Ripoti ya BBI kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta rasmi

Ripoti ya BBI kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta rasmi

Ripoti ya BBI kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta rasmi

Jopo la Upatanishi BBI litakutana na Rais Uhuru Kenyatta tarehe 26 mwezi Novemba kuwasilisha rasmi ripoti  ya BBI baada ya kukamilisha kuiandaa.

Amesema Mwenyekiti wa Jopo la BBI ambaye pia ni Seneta wa Wajir - Yusuf Haji.

Wakati wa Kikao na wanahabari Haji amesema hatua hiyo itakomesha mjadala tata iliyoibuliwa na wanasiasa kuhusu yaliyomo katika ripoti hiyo.

Amewashauri wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuhusu ripoti hiyo akiwashauri kupata taarifa rasmi kupitia barua pepe kwa anwani BBI@citizensupport.go.ke au katika mtandao wa Twitter @TheRealBBI.