array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yakakamikia kiwango cha chini cha bajeti
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mahakama yakakamikia kiwango cha chini cha bajeti

Mahakama yakakamikia kiwango cha chini cha bajeti

Idara ya Mahakama sasa imeiomba Seneti na Bunge la Kitaifa kutopitisha mapendekezo ya Wizara ya Fedha ya kupunguzwa kwa bajeti ikisema hatua hiyo itaathiri shughuli zote.

Msajili wa Mahakama Anna Amadi ameiambia Kamati ya Seneti ya Haki na Sheria kwamba huenda shughuli katika idara ya mahakama zikakwama ifikiapo Februari mwakani iwapo pendekezo hilo litatekelezwa. Amadi amesema miradi iliyokuwa imeanzishwa huenda ikakwama, kukashuhudiwa mrundiko wa kesi mahakamani vile vile kuathirika kwa mipango ya kuwaajiri majaji zaidi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Seneta wa Nandi Samson Cherargei ameihakikishia idara hiyo kuwa watalishawishi Bunge la Kitaifa kufutilia mbali mapendekezo hayo ya kupunguzwa kwa bajeti.

Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Jrn kwa upande wake ameishauri idara hiyo kufunga mahakama zote za ufisadi ili kulemaza juhudi za serikali za kukabili jinamizi hilo kwa lengo la kuishinikiza kutoa fedha.

Ikumbukwe Idara ya Mahakama ilikuwa imeomba kupewa shilingi bilioni 23, katika mwaka wa kifedha wa 2018/2019, ila ikapewa shilingi bilioni 18 ambazo sasa huenda zikapunguzwa kwa shilingi bilioni 3.3 iwapo mapendekezo ya Waziri Yattani yataidhinishwa.

Tayari Jaji Mkuu David Maraga amelalamikia hatua hiyo akiishtumu Serikali Kuu kwa kuwa na njama ya kulemaza shughuli za mahakama nchini.