array(0) { } Radio Maisha | Uchunguzi zaidi kufanyiwa mili ya watoto wa Joyce Syombua waliouliwa Nanyuki
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Uchunguzi zaidi kufanyiwa mili ya watoto wa Joyce Syombua waliouliwa Nanyuki

Uchunguzi zaidi kufanyiwa mili ya watoto wa Joyce Syombua waliouliwa Nanyuki

Mili ya Shanice Maua na Prince Michael waliouliwa pamoja na mama yao Joyce Syombua itafanyiwa uchunguzi zaidi kubaini iwapo walipewa dawa za kuwafanya walale kabla ya kunyongwa. Watalaam jana walichukua sampuli za wawili hao baada ya matokeo ya uchunguzi kutolewa na mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor kubaini kilichosabababisha mauaji yao.

Aidha licha ya kuwa mamaye marehemu Elizabeth Maua Malombe aliitambua mili hiyo uchunguzi zaidi wa DNA utahitajika kufanywa.

Akitoa ripoti hiyo, Oduor alisema kuwa mama yao Joyce aliuliwa kwa kupigwa mara kadhaa kichwani kwa kifaa butu na kutokwa damu nyingi kwenye ubongo wake huku wanawe wawili wakinyongwa. Aidha katika uchunguzi huo, alisema hangebaini siku hasa watatu hao waliuliwa kwani mili yao tayari ilikuwa imeanza kuoza.

<AUDIO>953

Hayo yanajiri huku mshukiwa mkuu wa mauaji hayo Peter Mugure ambaye pia ni mumewe Syombua akiendelea kuzuiliwa baada ya kufikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii ambapo mahakama iliagiza asalie rumande kwa siku ishirini na moja zaidi ili kutoa nafasi ya uchunguzi kufanywa.

Kwingineko mshukiwa mwingine wa mauaji hayo ambaye ni mfanyakazi katika kambi ya jeshi ya Nanyuki aliyetambuliwa kuwa Collins Pamba ameiambia mahakama kuwa alisaidai kuizika mili hiyo baada ya kuahidiwa kazi katika Idara ya Jeshi. Polisi wanasema katika ripoti ya mshukiwa kwao aliahidiwa kazi iwpao angeizika mili hiyo na kusalia kimya.