array(0) { } Radio Maisha | Man United taabani, madeni yaongezeka

Man United taabani, madeni yaongezeka

Man United taabani, madeni yaongezeka

Klabu ya Manchester United imeripotiwa na vyombo vya habari mapema jumatano, Uingereza ya kwamba ina deni la takriban pauni milioni 500.

Juhudi za Manchester united kuboresha kikosi chake kimewa gharimu pakubwa. Deni lao lilipanda kutoka asilimia 55 hadi pauni milioni 498 mwakani.

Wachezaji Harry Maguire, Aaron wan Bisaka na Daniel James waligharimu klabu hiyo tajika pauni milioni 140.

Naibu afisa mkuu mtendaji, Ed Woodward ameonesha imani na kuwaomba wote washika dau wa Manchester United wawe na subira.

“Nia yetu nikupunguza gharama ya kuwanunua wachezaji kwa kuboresha akademia yetu. Tuna vipaji ibuka vingi sana ambavyo vikikuzwa, klabu hii itarejesha hadhi yake barani Ulaya na Uingereza vile vile. Tunataka siku za usoni tucheze mchezo wa kutamanisha huku tukishinda mataji. Ili nia yetu itimie, itabidi tupunguze gharama ya kuwa nunua wachezaji tajika na kuwaamini makinda wa akademia,” alisema Woodward kwa matumaini.

Soko la hisa jijini New York, merekani lili rekodi mauzo ya pauni milioni 812 kutoka kwa klabu hiyo ya Manchester. Lakini mwaka wa 2019-20 una onekana kuwa mbaya kwa Man-U. inakisiwa klabu hiyo itaenda hasara ya kati ya pauni milioni 750 hadi 725.

Kumaliza kwa Manchester united katika nafasi ya sita msimu jana pia kumewaathiri pakubwa. Ina maanisha kwamba hela za kushirki klabu bingwa barani ulaya almaarufu kama Eufa champions league na hatimiliki za televisheni za msimu huu pia zimewatoka.

Manchester united kwa sasa inashikilia nafasi ya saba katika jedwali la ligii kuu uingereza, baada ya kucheza mechi 12, ina alama 16 pekee.

Jumapili hii vijana hao wa Olegunar watashuka dimbani ugenini Sheffield United, mechi ambayo kwamba wanatarajia kupata alama tatu na kujiboresha katika jedwali la ligii kuu uingereza katika hali ya kusaka tiketi ya nne bora ili kushiriki klabu bingwa barani ulaya msimu ujao.