array(0) { } Radio Maisha | Mhudumu wa bodaboda auliwa na afisa wa KDF Mombasa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mhudumu wa bodaboda auliwa na afisa wa KDF Mombasa

Mhudumu wa bodaboda auliwa na afisa wa KDF Mombasa

Mhudumu wa bodaboda eneo la Mtongwe kwenye Kaunti ya Mombasa ameuliwa kwa kupigwa risasi na maafisa wanaoaminika kuwa wa Jeshi la KDF muda mfupi uliopita.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, milio ya risasi imesikika mara kadhaa kabla ya mhudumu huyo anayedaiwa kuyavamia makazi ya maafisa hao yaliyo katika Kambi ya Jeshi ya Mtongwe Base kuuliwa.

Wakazi hawa ambao tumezibana sauti zao kwa sababu za itifaki wamekiambia kituo hiki kwamba baada mhudumu huyo kuuliwa mwili wake umekuwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa watatu. Baadhi ya wahudumu wa bodaboda ambao pia wameshuhudia mwenzao akiuliwa wamesema wanamfahamu afisa aliyetekeleza mauaji hayo.

Wanasema muhudumu huyo ameajiriwa na mmoja wa mafisa wa KDF kuendeleza shughuli hiyo ya uchukuzi wa bodaboda. Kufikia sasa, hakuna taarifa maalum ambayo imetolewa Idara ya Usalama kuhusu tukio hilo huku juhudi za kuwatafuta wakuu wa idara hiyo katika Kaunti ya Mombasa kwa njia ya simu zikiambulia patupu.