array(0) { } Radio Maisha | Mili ya Joyce Syombua na wanawe yatarajiwa kufanyiwa upasuaji

Mili ya Joyce Syombua na wanawe yatarajiwa kufanyiwa upasuaji

Mili ya Joyce Syombua na wanawe yatarajiwa kufanyiwa upasuaji

Mamaye Joyce Syombua, Elizabeth Malombe amefika katika Hifahi ya Maiti ya Nanyuki ambapo mili ya mwanawe na wajukuu wake imehifadhiwa.

Malombe anatarajiwa kuitambua mili hiyo kabla ya Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali, Johansen Oduor kuifanyia upasuaji.

Ikumbukwe mili ya Joyce Syombua na wanawe wawili ilipatikana Jumapili iliyopita ikiwa imezikwa katika makaburi ya Nanyuki.

Mshukiwa Mkuu wa mauaji ya watatu hao ambaye pia mumewe - Peter Mugure alifikishwa mahakamani Jumatatu ambapo mahakama iliagiza aendeleee kuzuiliwa kwa siku ishirini na moja ili kutoa nafasi kwa uchunguzi kufanywa.