array(0) { } Radio Maisha | Nina matumaini ya kurejea uwanjani rasmi, mapema Januari; Otieno
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Nina matumaini ya kurejea uwanjani rasmi, mapema Januari; Otieno

Nina matumaini ya kurejea uwanjani rasmi, mapema Januari; Otieno

Beki mahiri wa pembeni kulia timu ya taifa Harambee Stars na Gormahia, amewapa matumaini mashabiki wa kandanda nchini kwa kusema kwamba ana matumani ya kurejea uwanjani mapema Januari mwaka ujao.

Philemon Otieno, almaarufu kama ‘Mbish’ mitaani Babadogo, Kaunti ya Nairobi, alizungumza na meza ya michezo Redio Maisha mapema jumanne.

“ Nimekuwa napokea matibabu pole pole. Kwa sasa nimeanza mazoezi mepesi. Goti langu ambalo lilifanyiwa upasuaji kwa sasa limeanza kupata nafuu. Nina tembea vizuri na hata kukimbia pole pole. Kilicho salia tu sasa nikuuzoesha mguu wangu tena kucheza mpira,” mchangamfu huyo Philemon alizungumza.

Mbish alijeruhia akiichezea timu ya taifa Harambee Stars katika michuano ya kuwania ubingwa wa barani Afrika, wachezaji wa ligii za ndani ‘CHAN’. Katika mechi hiyo, Harambee stars ilibanduliwa nje ya mashindano na Taifa Stars ya Tanzania.

“Jeraha hili sikulipata wakati wa michuano ya barani Afrika AFCON kama wengi wanavyodhania. Huko nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuichezea timu ya taifa japo mambo yalituendea upogo. Baada ya kujeruhiwa, ilichukua takriban mwezi mmoja kabla nianze matibabu. Ukweli ni kwamba sikuwa na shilingi nusu milioni ambazo zilihitajiwa kugharamia upasuaji na matibabu kwa ujumla. Pia nahitaji shilingi elfu nne mia tano kila wiki kuhudhuria matibabu na ukaguzi wa goti langu. Goti hili hutibiwa mara tatu kwa wiki.” Alisema beki huyo wa Gormahia huku akiongezea kwamba marafiki wake na familia yake walimsaidia pakubwa kifedha wakati alipowahitaji.

Beki huyo ambaye alikuwa nahodha wa Ushuru fc kabla ya kujiunga na mabingwa mara 18 wa KPL Gormahia, mapema mwezi wa Septemba alilalamika ya kwamba ametelekezwa na shirikisho la kandanda nchini FKF baada ya jeraha lake. Aliwaomba wahisani wajitokeze na kumsaidia.

“Sitaki kuongelea mengi kuhusu yaliyotokea maanake yashamwagika, hatuwezi kuyazoa. Kilicho muhimu sasa ni mimi kumakinikia matibabu na mazoezi. Nina matumaini Januari mwaka ujao, nitashuka tena dimbani.” Alitabasamu Philemon.

Philemon Otieno ni mchezaji ambaye kwamba ana ndoto na matumaini ya kushinda ligi tena na Gormahia na kisha baadae acheze barani Ulaya kabla ya kustaafu. Ndoto yake nusura ikatizwe na jeraha la goti lakini marafiki wake walimsaidia. Sasa ana matumaini ya kurejea uwanjani mwaka ujao na kuendelea kutamba huku akiipeperusha bendera ya Kenya na klabu yake Gormahia.