array(0) { } Radio Maisha | Watu watano wafariki dunia kwenye ajali eneo la Man Eaters, Tsavo

Watu watano wafariki dunia kwenye ajali eneo la Man Eaters, Tsavo

Watu watano wafariki dunia kwenye ajali eneo la Man Eaters, Tsavo

Idadi ya watu waliofariki dunia kufuatia ajali kwenye eneo la Man Eaters mjini Voi, imefikia watano.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema gari la kuwabeba abiria liliugonga upande mmoja wa trela wakati dereva alipokuwa akijaribu kulipita.

Mili imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Voi huku waliojeruhiwa wakiendelea kutibiwa katika hospitali iyo hiyo.

Idara ya polisi kwenye Kaunti ya Taita Taveta imewashauri wanaotumia barabara hiyo kuwa makini ikizingatiwa ni telezi wakati huu mvua inanyesha.

Awali idara ya trafiki kwenye kaunti hiyo iliwatahadharisha wahudumu wa magari kuwa makini kati ya eneo la Mtito na Maungu, kwa kuwa sehemu hizo ni hatari, kwani ajali nyingi zimekuwa zikiripotiwa sehemu hiyo.