×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Victor Wanyama chini ya Jose Mourinho, Spurs

Victor Wanyama chini ya Jose Mourinho, Spurs

Aliyekuwa meneja wa klabu ya  Man United na Chelsea Jose Mourinho ametia saini kandarasi hadi mwisho wa msimu wa mwaka 2022-23.

Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy amesema ''Jose ni mmojawapo wa wakufunzi waliofanikiwa sana katika soka na kuboresha vilabu'',

Jose Mourinho alidaiwa kuwa katika mazungumzo ya kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino kama mkufunzi wa Tottenham.

Pochettino mwenye umri wa miaka 47 alifutwa kazi ya umeneja Spurs Jumanne baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano akiisimamia klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Raia huyo wa taifa la Argentina aliiongoza Spurs katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita ambapo walipoteza baada ya kutandikwa na Liverpool ambayo inaongozwa na Jurgen Klop.

Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amekuwa bila kazi ya ukufunzi tangu alipofutwa kazi na United mnamo Disemba 2018 na klabu ya Manchester United.

Kumekuwepo na ripoti kuhusu mkwaruzano kati ya Pochettino na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy , lakini uamuzi huo ulichukuliwa kutokana na msururu wa matokeo duni katika kipindi cha miezi kadhaa , kuanzia Februari mwaka 2019 .

Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe, kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann na aliyekuwa kocha wa Juventus Masimilliano Allegri wote wamehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Spurs.

Baadhi ya maafisa katika klabu hiyo wanaendelea kuwa na matumaini kwamba Mourinho huenda akazinduliwa katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Alhamisi iwapo mazungumzo yatakamilika vizuri.

Spurs haijawahi kumsajili meneja aliye na mahitaji ya kiwango cha juu zaidi kama Mourinho , na wala haijawahi kutumia fedha nyingi kuwanunua wachezaji kama vile alivyozoea katika klabu za Real Madrid na Man United.

Hivyo basi mashabiki wengi watashangazwa kwamba huenda akajiunga na klabu hiyo huku kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsman akionekana kijana zaidi na mwenye uwezo wa kuongoza klabu hiyo.

Lakini Spurs katika miaka ya hivi karibuni wametoka mbali chini ya ukufunzi wa Pochettino .

Spurs Wana uwanja mpya uliojengwa kwa thamani ya pauni bilioni moja na uwanja wa mazoezi mbali na kufuzu kushiriki katika ligi ya mabingwa mara nne mfululizo huku