array(0) { } Radio Maisha | Sina ubaya na Sofapaka, Jukumu la mwajiri ni kumlipa mwajiriwa; Asike
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sina ubaya na Sofapaka, Jukumu la mwajiri ni kumlipa mwajiriwa; Asike

Sina ubaya na Sofapaka, Jukumu la mwajiri ni kumlipa mwajiriwa; Asike

Beki kati wa klabu ya Tusker fc Eugine Asike ameiomba radhi Sofapaka fc mapema jumatano, huku akisisitiza ya kwamba tukio la mwaka wa 2015 lilikuwa ni hali ya kazi.

Akizungumza baada ya mazoezi ya klabu hiyo uwanjani Ruaraka kaunti ya Nairobi, Asike pia alisisitiza umuhimu wa wachezaji wakenya kujua haki zao.

“Kuna shida kubwa sana nchini Kenya haswa ukiangazia vilabu ambavyo vinashiriki KPL. Shida ambayo nilikuwa nayo Sofapaka si yangu pekee. Kuna wengi wachezaji nchini ambao wanadhulimiwa na vilabu vyao lakini hawazungumzi kwa sababu ya kudhalilishwa,” alisema Asike huku akiongezea kwamba hatua ya kuishtaki klabu ya Sofapaka fc ilikuwa niya ujasiri mno na pia ya kuwaelimisha wenzake wachezaji kuhusu haki zao.

Asike aliichezea Sofapaka fc msimu wa 2014/2015. Ukuruba wake na ‘Batoto ba Mungu’ uliingia donda wakati alijeruhiwa huku mshahara wake pia ukicheleweshwa.

“Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu. Sofapaka haikunilipa mshahara miezi mitatu. Ilinibidi nichukue hatua na kwenda kortini. Ni kweli nilikuwa na wakili ambaye alinisaidia kuwasilisha kesi yangu na hatimaye nikapata haki baada ya vute niku vute kati ya mimi na mwajiri wangu wa wakati huo Sofapaka,” Asike alinena kwa matumaini huku akiwarai wachezaji wenzake kuwa na ujasiri wa kuzungumza na pia watumie mawakili wa michezo.

Wakili wake wakati huo Elvis Majani, aliwasilisha kesi hiyo mahakamani na kupata ushindi ambao ulisifiwa pakubwa na rais wa chama cha haki za wachezaji kandanda duniani ‘Fifpro’ Andrew Orsatti.

“Sofapaka haikumlipa mteja wangu miezi mitatu mwisho wa mwaka 2014. Pia ikumbukwe ya kwamba, klabu hiyo haikumlipa ada ya usajili ambayo walikuwa wamekubaliana kwa mkataba. Kwa hivyo walikuwa na kesi ya kujibu,” Majani alitabasamu huku akiongezea kwamba wachezaji wengi nchini Kenya wanadhulimiwa huku wakiendelea na maisha yao kimya kimya.

Eugine Asike ambaye kwa sasa ana kaba safu ya ulinzi ya Tusker fc, ana matumaini ya kurejea katika timu ya taifa Harambee Stars. Francis Kimanzi, mwaka wa 2012 alimpa nafasi baada ya Pascal Ochieng kujeruhiwa.

Kimanzi sasa amerejea kuifunza timu ya taifa kwa mara ya tatu, na beki huyo wa zamani wa Kcb, Sofapaka na sasa Tusker fc ana matumaini ya kwamba alicho kiona wakati ule wa 2012 Kimanzi alipomchagua, atakiona tena wakati huu.