array(0) { } Radio Maisha | TSC yaorodhesha majina ya watakaowania nyadhifa katika tume hiyo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

TSC yaorodhesha majina ya watakaowania nyadhifa katika tume hiyo

TSC yaorodhesha majina ya watakaowania nyadhifa katika tume hiyo

Tume ya Huduma za Walimu, TSC imeorodhesha majina ya watu ishirini na wanne watakaohojiwa katika nyadhifa za wanachama wa tume hiyo. Shughuli ya kuwahoji itaanza tarehe 25 mwezi huu na kukamilika tarehe 27.

Wakati uo huo, Mwenyekiti wa Jopo la Uteuzi wa watu hao - John Munene Njenga amesema walio na malalamiko kuhusu yeyote ambaye ametuliwa kuwasilisha malalamiko yake ifikiapo tarehe 22 mwezi huu yaani siku ya Ijumaa.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Profesa Maurice N. Amutabi, Flora, Mutuweta, Dkt. Cleophas Ondiek, Leila Abdi Ali, Florence Wajiku Njau, Mary Rotich, Bardad Adow Mohammed, Dorothy, Kimeu na Lilian Nyambura Wachira.

Wengine ni Mohamud Kasai, Margaret Iyasi Lesuuda, Pius, Nduath, stephen Nthiga Mitugo, Mbage, Njuguna Ng'ang'a Mukulu Ngilu, Amina Hassan Ahmed miongoni mwa wengine.

Ikumbukwe mwezi Septemba mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta alimteua Munene kiongoza jopo la watu tisa ambalo limejukumiwa kuwateua makamisha wa TSC baada ya muda wa kuhudumu wa watatu wao kukamilika. Makamisha ambao muda wao umekamilika ni Cleophas Tirop, Salome Gichura na Saadia Abdi Kontoma. Aidha, Muda wa Kuhudumu wa Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Machari unatarajiwa kukamilika mwakani ila anaruhusiwa kutuma maombi kwa kipindi kingine.