array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta leo ameteketeza silaha 8700 haramu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Uhuru Kenyatta leo ameteketeza silaha 8700 haramu

Rais Uhuru Kenyatta leo ameteketeza silaha 8700 haramu

Rais Uhuru Kenyatta leo ameteketeza silaha 8700 haramu na zaidi ya  vifaa vingine elfu 366 vinvyotumika na wahalifu zikiwamo risasi katika Chuo cha Mfunzo ya GSU cha Magadi, Kaunti ya Kajiado. Rais amesema hatu hiyo ni kudhihirisha utayarifu wa serikali kutumia kila mbinu ili kuwalinda raia wake dhidi ya wahalifu na raia wenye silaha haramu.

Rais amesisitiza haja ya Wakenya kufuata taratibu zilizowekwa ikiwa wanataka kujihami kupitia Bodi ya Kutoa Leseni huku akisema tayari serikali imeweka sajili ya kidijitali ili kuwatambua wote walio na silaha hizi na ni rahisi kutumia sajili hiyo ili kuwakabili wnaaotumia silaha isivyofaa.

Kuhusu suala ambalo limegeuka donda ndugu la wizi wa mifugo, Rais amewataka viongozi wa jamii kuongoza katika mikakati ya kuwahamisha wakazi kusalimisha silaha na kuacha hulka hiyo.

Akizungumza katika hafla hiypo, Wazieri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Dkt Fred Matiang'i amesema zaidi ya silaha 130 zimetwaliwa kutoka  kwa mikono ya raia katika operesheni ya hivi punde zaidi. Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai, Waziri wa Mazingira Keriao Tobiko na Mwanasheria Mkuu wa serikali, Keriako Tobiko ni miongoni mwa waliohudhuria.