array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Embrace, wasisitiza amani kabla ya kutolewa kwa ripoti ya BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa Embrace, wasisitiza amani kabla ya kutolewa kwa ripoti ya BBI

Viongozi wa Embrace, wasisitiza amani kabla ya kutolewa kwa ripoti ya BBI

Huku ripoti ya Jopo la Upatanishi BBI ikitarajiwa kuwasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga, kundi la viongozi wa Kike wanaounga mkono mwafaka kati ya viongozi hao wawili, la Embrace limesisitiza haja ya kuwapo kwa amani na umoja nchini ripoti hiyo ikisubiriwa kuwekwa wazi.

Wakirejelea uchaguzi wa mdogo wa Kibra, viongozi hao wanaowajumuisha magavana, wabunge vilevile maseneta wameeleza kuridhishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa. Aidha, wamewakashifu viongozi wenza wa kundi la Inua Mama na Tangatanga ambao wamekuwa wakidai kuwa viongozi wa ODM walisababisha vurugu katika uchaguzi huo.

Wakati wa kikao na wanahabari, Gavana wa Kirinyanga Ann Mumbi, amesisitiza kwamba mwafaka kati ya Rais Kenyatta na Raila Odinga umechangia kuwapo kwa amani nchini. Amewashauri viongozi nchini kusitisha siasa za migawanyiko na mirengo na badala yake kuunga mkono mwafaka baina ya Uhuru na Raila wa mwezi Machi mwaka jana vilevile Jopo la BBI.

 

Mbunge wa Likoni, Mishi Mboko kwa upande wake amesisitiza kwamba wana matumaini kuwa ripoti ya BBI itayajumuisha maoni ya kundi la Embrace yaliyopigia debe kuwapo kwa usawa wa uwakilishi katika uongozi vilevile kubuniwa kwa nafasi zaidi za uongozi serikalini.