array(0) { } Radio Maisha | Mahakama imepuuza ombi la Jasusi wa binafsi Jane Mugo kutaka alindwe

Mahakama imepuuza ombi la Jasusi wa binafsi Jane Mugo kutaka alindwe

Mahakama imepuuza ombi la Jasusi wa binafsi Jane Mugo kutaka alindwe

Mahakama Kuu ya Milimani, imepuuza ombi la Jasusi wa binafsi Jane Mugo kutaka alindwe na serikali.

Mugo katika ombi lake,  ameiomba mahakama iagize serikali impe ulinzi wa kutosha wakati wa uchunguzi na kusikilizwa kwa kesi ambapo anatuhumiwa kuwatishia maisha watu wawili.

Hata hivyo, Jaji Martha Mutuku amekataa ombi hilo kwa msingi kwamba Mugo ameshindwa kuielezea mahakama ni kwanini angependa alindwe na serikali.

Mwezi uliopita , Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP Nordin Hajii aliiagiza mahakama kumzuilia Mugo katika Gereza la Wanawake ya Lang'ata na kuhakikisha kuwa yu salama baada ya kudai kuwa maisha yake yamo hatarini.

 Upande wa Mashtaka katika kesi hiyo,  umesema kuwa Mugo ataendelea kuzuiliwa katika gereza hilo ambapo kuna usalama wa kutosha .
 
Kupitia wakili wake Danstan Omari na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Kiambu Brian Khaemba, Mugo amesema ni kwa neema ya Mungu ambapo yuko hai leo hii.
 
Ikumbukwe mwezi uliopita Mugo kupitia cheti kiapo alisema kuwa maisha yake yametishiwa na baadhi ya maafisa wanaochunguza kesi dhidi yake.
 
Mugo aidha alisema kuwa licha ya kuripoti vitisho dhidi yake kwa polisi  tangu mwaka wa 2014, hakuna hatua yoyote imechukuliwa.