array(0) { } Radio Maisha | Mtahiniwa wa KCPE amemshukuru mhudumu wa bodaboda kwa kufanikisha elimu yake

Mtahiniwa wa KCPE amemshukuru mhudumu wa bodaboda kwa kufanikisha elimu yake

Mtahiniwa wa KCPE amemshukuru mhudumu wa bodaboda kwa kufanikisha elimu yake

Mtahiniwa wa KCPE Ashley Akinyi wa Shule ya Binafsi ya Light Academy Mombasa aliyejizolea alama 416 amechukua fursa ya kipekee kumshukuru mhudumu wa bodaboda aliyekuwa akimsafirisha hadi shuleni.

Mbali na kushukuru ushirikiano baina ya walimu na wazazi, anasema mhudumu huyo kwa jina Kevin Njoroge maarufu Tyson alijitolea kuhakikisha anafika shuleni kwa wakati.

Amesema Tyson alikuwa akirauka asubuhi na mapema na kumsafirisha kutoka nyumbani kwao Bamburi hadi shuleni kwa takriban kilomita tano.

Tumefanikiwa kumpata Tyson anayehudumu eneo la Masters Bamburi ambaye amemtaja kuwa msichana mpole aliyependa elimu yake.

Tyson amesema wakati umefika kwa umma kujitenga na dhana kwamba wahudumu wa bodaboda si watu wa kuaminika kwani pia wanachangia pakubwa katika ufanisi wa watu mbalimbali.

Amewahimiza wenzake kutekeleza majukumu yao kikamilifu.