array(0) { } Radio Maisha | Riccini amefutwa kazi baada ya kuwashinda wapinzani 27-0
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Riccini amefutwa kazi baada ya kuwashinda wapinzani 27-0

Riccini amefutwa kazi baada ya kuwashinda wapinzani 27-0

Paulo Brogelli, Rais wa Klabu ya Invicta Sauro, Tuscany, Italia amemfuta kazi meneja wake wa vijana wasiozidi umri wa miaka 18 baada ya kupata ushindi mnono wa 27-0 mapema jumapili.

Akizungumza na vyombo vya habari kule Italia mapema leo hii baada ya mechi yao dhidi ya Marina Calcio, Brogelli alionesha ukali.

“Nimesikitishwa sana na matokeo ya leo. Nimeshangazwa sana na jinsi kocha mkuu Masimilliano Riccini alivyo wadharau wapinzani wetu. Mchezo wa kandanda niwa heshima na zaidi ya yote uhamasisho. Haya mambo hayakutokea leo wakati chipukizi wetu walipo chuana na Marina,” alifoka Brogelli.

Rais huyo pia aliongezea kwamba klabu yake ina filosofia ya kuwafunza chipukizi itikadi za maisha, kuwaheshimu wapinzani na zaidi ya yote kuwa na utu.

“Mambo haya ambayo tunawafunza vijana hawa, hatuku ya shuhudia leo. Masimilliano Riccini basi amefeli majukumu yake kama mkufunzi. Hatutaki kuwa na uhasama na wenzetu maanake tunahitajiana kila uchao. Mimi pamoja na bodi ya klabu hii, tunaomba msamaha kwa wapinzani wetu,” alisema Brogelli.

Invicta Sauro ikiongozwa na rais Brogelli, walifanya kikao cha dharura na bodi ya klabu hiyo baada ya mechi hiyo. Wote kwa pamoja walikubaliana ya kwamba Riccini afutwe kazi. Kisa na maana; amekosa heshima kwa wapinzani.

Basi kama mambo ndio hivi kule bara ulaya, si ajabu vilabu kama Arsenal na Tottenham hotspurs za Uingereza bado hazijawafuta kazi makocha wao. Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni.