array(0) { } Radio Maisha | Wetangula awataka Wakenya kuwa na subira na ripoti ya BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wetangula awataka Wakenya kuwa na subira na ripoti ya BBI

Wetangula awataka Wakenya kuwa na subira na ripoti ya BBI

Kinara wa Chama cha FORD Kenya, Moses Wetangula amesema ripoti ya Jopo la Upatanishi, BBI haifa kuchukuliwa kama ya viongozi wawili, Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga. 

Akihutubu wakati wa mazishi ya baba ya aliyekuwa seneta wa Kaunti ya Trans Nzoia,  Henry Ole Ndiema, Musa Kigai Ndeima, Wetangula amewasihi wanaoikosoa ripoti hiyo kusubiri hadi wakati itakapotolewa wazi kwa umma.

Kwa upande wao Mbunge wa Endebess , Daktari Robert Pukose na mwenzake wa Kimilili, Didmus Barasa wamesema wataipinga ripoti ya BBI ikiwa inalenga kubuni nyadhifa zaidi za  uongozi na kukosa  kuongezwa raslimali katika serikali za kaunti.

Waziri wa Ugatuzi , Eugene Wamalwa amewahakikishia Wakenya kwamba serikali itayatilia maanani maoni yao kabla ya kuitekeleza ripoti hiyo.