array(0) { } Radio Maisha | KNUT na COTU zatangaza kuunga mkono ripoti ya BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

KNUT na COTU zatangaza kuunga mkono ripoti ya BBI

KNUT na COTU zatangaza kuunga mkono ripoti ya BBI

Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT na Muungano wa Vyama vya Wafanyikazi Nchini COTU umetangaza rasmi kuunga mkono Ripoti ya Upatanisho BBI huku Mbunge wa Cherangany Joshua Kutuny akitangaza msimamo kuwa haungi mkono mrengo wowote wa kisiasa nchini.
 

Akihutubu kwenye hafla ya kuchangisha pesha katika Kanisa la Evangelical Bible Church mjini Eldoret Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema kuwa pana haja ya katiba kufanyiwa marekebisho kama njia moja ya kuwaunganisha Wakenya.
 
Kwa mujibu wa Atwoli Jopo la BBI linalenga kuhakikisha kuwa taifa hili halishuhudiii machafuko baada ya uchaguzi.
Aidha ametangaza kuwa na imani kuwa iwapo kura ya maoni itafanyika ili kuidhinisha mapendekezo ya BBI Wakenya watayapitisha.
 

Kwa upande wake Katibu Mkuu KNUT Wilson Sossion amesema kuwa chama hicho kimeshiriki mazungumzo na wanachama wake na kuafikiana kwamba kitaunga mkono mapendekezo ya BBI.

Aidha KNUT itaendelea kushirikiana na Rais Uhuru Kenyatta na kumuunga mkono kwa kila jambo.
Amewataka viongozi kutopinga mapendekezo ya BBI badala yake kusaidia katika kurekebisha vipengele ambavyo vitaonekana kuwa na utata

 

Kauli yake imeungwa mkono na  Mbunge wa Cherang’any Joshua Kutuny akisema kuwa katiba ya sasa inazibagua baadhi ya jamii nchini na kuzinufaisha jamii mbili tu ambazo zimekuwa zikiliongoza taifa tangu jadi.