array(0) { } Radio Maisha | Mili inayoaminika kuwa ya mama na wanawe waliyoripotiwa kutoweka yapatikana Nanyuki
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mili inayoaminika kuwa ya mama na wanawe waliyoripotiwa kutoweka yapatikana Nanyuki

Mili inayoaminika kuwa ya mama na wanawe waliyoripotiwa kutoweka yapatikana Nanyuki

Maafisa wa uchunguzi wameifukua mili  inayoaminika kuwa mama na wanawe wawili waliotoweka wiki tatu zilizopita kwenye eneo la Nanyuki Kaunti ya Laikipia baada ya kumtembelea Peter Mwaura afisa wa Jeshi wa Laikipia Airbase.

Kwa mujibu wa Afisa aliyenaendesha uchunguzi huo Muinde Mwau, ni kwamba watafanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kuwa mili iliyofukuliwa ya mwanamke huyo na wanawe waliotoweka.

Afisa huyo aidha ameongeza kuwa walielekezwa na mshukiwa huyo eneo walikozika mili hiyo na muda tu baada ya kufika eneo hilo wakaipata mili hiyo. Wakazi wa eneo la Nanyuki vilevile wametoa maoni yao kuhusu kisa hicho cha mauaji.

Joyce Wambua alimtembelea mumewe Peter Mwaura kutoka Nairobi hadi Nanyuki tarehe ishirini na sita na siku iliyofuata wakatoweka. Hata hivyo simu ya Joyce ilipatikana kwenye gari la abiria ikidaiwa kuwa ilikuwa njama ya kupoteza ushahidi wa mauaji hayo.