array(0) { } Radio Maisha | ''Tumekuwa walevi chakari baada ya kustaafu, kwa sababu hatukufunzwa kujipanga'' amesema Noah Ayuko
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

''Tumekuwa walevi chakari baada ya kustaafu, kwa sababu hatukufunzwa kujipanga'' amesema Noah Ayuko

''Tumekuwa walevi chakari baada ya kustaafu, kwa sababu hatukufunzwa kujipanga'' amesema Noah Ayuko

Aliyekuwa mlinda lango wa zamani Timu ya Taifa Hambee Stars Noah Ayuko, amehimiza Shirikisho la Kandanda nchini FKF kujumuisha mafunzo kuhusu maisha katika mchezo wa kandanda.

Akizungumza na Redio Maisha idara ya michezo Jumamosi kiwa Naivasha mjini, Ayuko amejutia  maisha yake baada ya kustaafu.

“ Nimechezea vilabu tofauti tofauti maishani mwangu ambavyo vilikuwa mashuhuri kama vile Oserian Fastac wakati ule. Hela hazikuwa shida nilipokuwa nikicheza, hata timu ya taifa wakati wetu pia tulilipwa vizuri. Nilikuwa mtu mashuhuri sana wakati huo na kila mtu alitamani kuwa karibu na mimi. Shida za maisha kama haya hutokea wakati umestaafu ama kuna uchache wa hela. Hapo basi nilijipata na msongo wa mawazo, kisha pombe ikawa rafiki yangu,” alikiri Ayuko huku akionekana kwamba bado hajapata utimamu wa mwili na utulivu wa akili. Ayuko pia aliongezea kwamba shida za maisha ndizo zimemfanya kuingilia pombe haramu kwa sababu inapatikana kwa urahisi na bei nafuu.

Asilimia kubwa ya wachezaji wa zamani nchini Kenya wamesakamwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya ugumu wa maisha na hali mbovu ya uchumi. Idara ya Michezo serikalini na shirikisho la kandanda FKF hazijawekeza ipasavyo katika vilabu vya kandanda.

“ Wachezaji ambao tulikuwa tunacheza nawo mechi za kimataifa kutoka nchi jirani kama vile Uganda, Ethiopia, Tanzania na kwingineko wana maisha mazuri. Serikali za kwao zimewekza katika vilabu. Wakuu wa vilabu nawo wamehakikisha wachezaji wao wame elimika. Wengi wetu waliochezea timu ya taifa Hambee Stars, tume athirika na janga hili la ulevi chakari kwa sababu hatukufunzwa jinsi ya kuwekeza hela zetu na pia kutunza maisha yetu ya kesho,” alijutia Ayuko huku akiionya FKF ya kwamba iwapo haitawekeza katika mafunzo ya itikadi za maisha, basi wachezaji wakenya wataishia kupotelea katika madanguro ya pombe vijijini na mitaani.

Naibu Rais FKF Bi. Doris Petra pia amekiri kwamba shirikisho bado halijawa na mikakati maalum ya mafunzo haya lakini utaratibu unaandaliwa pole pole.

“ Ni kweli kwamba jambo hili nila kusikitisha. Japo pia wachezaji wenyewe ndio wakulaumiwa kwa sababu wengi wao hujitosa katika maisha ya anasa bila kujali maisha yao ya kesho. FKF sasa tuna mpango wa kuwa na vikao vya elimu kwanzia mashinani. Vikao hivi vitawajumuisha wataalam ambao watawafunza wachezaji wa sasa, waliostaafu na hata wale wa kesho jinsi ya kuwekeza.” Petra aliongeza matumaini.

Nchini Kenya, wachezaji wengi wa zamani wamekumbwa na matatizo ya ulevi. Si Noah Ayuko peke yake, yeye ni mmoja kati ya ma elfu ambao sisi hatuwajui. Hali ngumu ya maisha na uchumi imeathiri mchezo wa kandanda kwa ujumla. Vilabu vya kandanda havina hela, ligii kuu KPL imekosa dhamani na wasimamizi wa kandanda hawaja ajibika ipasavyo katika uwekezaji wa mchezo huu nchini Kenya kwa ujumla.

Noah Ayuko kwa sasa ni mkufunzi wa chipukizi na ana matumaini ya kwamba iwapo mchezo wa kandanda nchini Kenya utakuzwa ipasavyo, basi swala la elimu nalo litiliwe mkazo. Mchezaji ambaye ame elimika ni bora katika utekelezaji wa maamuzi kuliko  yule ambaye hana elimu ama ana elimu duni.