array(0) { } Radio Maisha | Francis Wangusi kuendelea kuhudumu CA
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Francis Wangusi kuendelea kuhudumu CA

Francis Wangusi kuendelea kuhudumu CA

Na Victor Mulama,

NAIROBI, KENYA, Francis Wangusi ataendelea kuhudumu kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano, CA hadi bodi nyingine itakapobuniwa kwa kuzingatia sheria, imesema Mahakama ya Uajiri na Leba.

Jaji wa mahakama hiyo, Byron Ongaya ametoa uamuzi huo huku akifutilia mbali uteuzi wa wanachama kumi na watatu wa Bodi ya CA.

Ongaya aidha amebatilisha uteuzi wa Mercy Wanjau, ambaye alikuwa ameteuliwa kikaimu kujaza nafasi ya Wangusi baada ya muda wake wa kuhudumu kukamilika.

Mahakama vilevile imemwagiza Wangusi kuendelea kuhudumu hadi pale bodi nyingine itakapoteuliwa huku imtaka Rais Uhuru Kenyatta  kutumia mamlaka yake kuongeza muda wa kuhudumu kwa Wangusi hadi bodi mpya itakapobuniwa.

Jaji Ongaya, amesema kuwa Waziri wa Mawasiliano na Technologia Joe Mucheru, hana mamlaka ya kumteua mrithi wa Wangusi, akitaja uteuzi wa Wanjau kuwa uliokiuka sheria.  Wanjau aliteuliwa Agosti mwaka huu kujaza nafasi ya  Wangusi ambaye alianza kuhudumu mwaka wa 2012.

Uamuzi wa mahakama umefuatia ombi lililowasilishwa na Wakili, Henry Kurauka wa Chama cha Kutetea Maslahi ya Wateja, Cofek na Mwanaharakati, Okiya Omtatah la kutaka bodi hiyo ivunjwe kwa misingi kwamba sheria zinazosimamia utendakazi wa bodi hiyo zina kasoro.

Hata hivyo, Bodi ya CA kupitia wakili Githu Muigai, imesema kuwa Wangusi aliondolewa afisini kwa mujibu wa sheria, baada ya muda wake kukamika huku ikipinga kauli ya mahakama kuwa Mwenyetiki Ngene Gituku, alimzuia kuingia afisini ili kufanikisha uteuzi wa Wanjau.