array(0) { } Radio Maisha | Baadhi ya viongozi wazuiliwa kuhudhuria mkutano wa Rais

Baadhi ya viongozi wazuiliwa kuhudhuria mkutano wa Rais

Baadhi ya viongozi wazuiliwa kuhudhuria mkutano wa Rais

Na Victor Mulama,

NAIROBI, KENYA, Baadhi ya viongozi waliofika kwenye mkutano wa Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wa eneo la kati unaoendelea katika Ikulu ya Sagana kwenye Kaunti ya Nyeri, wamefungiwa nje huku wakilalamikia kuzuiliwa kuingia licha ya kufika mapema.

Viongozi hao wamesema walitakiwa kuweka simu zao kwenye gari japo baada ya kufika katika lango la Ikulu wakazuiliwa kuingia ndani.

Viongozi hao aidha wameeleza kuwa licha ya kutoka maeneo mbali kama mjini Eldoret wamezuiliwa nje hata baada ya kuwa katika sajili ya majina ya waliofaa kuhudhuria mkutano huo.

Kwa mujibu wa sheria, rais anapowasili katika hafla yoyote hakuna kiongozi yeyote anaekubaliwa kuingia baadaye.