array(0) { } Radio Maisha | Wakili Murgor aondolewa katika orodha ya viongozi wa mashtaka ya umma

Wakili Murgor aondolewa katika orodha ya viongozi wa mashtaka ya umma

Wakili Murgor aondolewa katika orodha ya viongozi wa mashtaka ya umma

Na Caren Omae,

NARIOBI, KENYA, Hatimaye Wakili Philip Murogor ameondolewa katika orodha ya viongozi wa mashtaka ya umma nchini. Katika taarifa ambayo imechapishwa katika gazeti rasmi la serikali Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP Noordin Haji amemwondoa Murgor ambaye alijuzulu wadhfa huo mwaka jana.

Ikumbukwe nafasi yake katika ofisi hiyo ya DPP iliibua mjadala mkali mahakamani wakati wa kesi ya mauzji ya bilionea Tob Cohen, ambapo upande wa mashtaka ulipinga aendelee kumwakilisha mshukiwa mkuu Sarah Cohen.

Mawakili wa ndugu za Cohen wakiongozwa na Cliff Ombeta walipinga hatua ya Murgor kuendelea kumwakilisha Wairiimu kutokana na nafasi hiyo.

Hata hivyo, Jaji Stella Mutuku aliamuru kwmaba Murgor ataendelea kumwakilisha Wairimu kwani tayari alikuwa amejiuzulu wadhfa huo, na kuwa hakukuwa na mwilingilio wa majukumu ilivyokuwa imedaiwa awali.

Wairimu anatuhumiwa kumuua mumewe, Cohen kisha kuutupa mwili wake katika tanki la maji taka katika makazi yao yaliyoko mtaani Kitusuru.