array(0) { } Radio Maisha | Ni vigumu kusafiri kwa zaidi ya saa mbili nje ya mazingira ya ndege
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ni vigumu kusafiri kwa zaidi ya saa mbili nje ya mazingira ya ndege

Ni vigumu kusafiri kwa zaidi ya saa mbili nje ya mazingira ya ndege

Na Mate Tongola,

NAIROBI, KENYA, Ni vigumu kwa binadamu kusafiri kwa zaidi ya saa mbili nje ya mazingira ya ndege kutokana na ukosefu wa okjeni inayopatikana ndani ya chombo hicho cha usafiri.

Kwa mujibu wa mtandao wa Google, ndege zinazosafiri zaidi ya umbali wa kilomita mia tano, hustahili kupaa zaidi ya futi elfu thelathini na tano ambayo ni juu ya mawingu.

Aidha, mtandao huo umearifu kwamba hali ya anga hubadilika pakubwa baada ya mita elfu mbili kutoka ardhini na hivyo kuwa vigumu kwa kiumbe chochote kustahimili upepo makali pamoja na nyusi zaidi ya -60.

Maelezo haya yanafafanua hali iliyomkumba mkenya Paul Manyasi aliyesafiri kisiri kwa ndege ya Kenya Airways kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuelekea Heathrow, Uingereza - umbali wa kilomita elfu nne, mia mbili hamsini na mbili.

Aidha, huenda Manyasi alifariki dunia akiwa angani kutokana na upepo mkali, ukosefu wa okjeni na kijibaridi, hata kabla ya mwili wake kuanguka baada ya ndege hiyo kujitayarisha kutua.