array(0) { } Radio Maisha | Uhuru kukutana na viongozi wa Mlima Kenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Uhuru kukutana na viongozi wa Mlima Kenya

Uhuru kukutana na viongozi wa Mlima Kenya
Na Caren Omae,
NAIROBI, KENYA, Madai kwamba Rais Uhuru Kenyatta ameshindwa kutoa mwelekeo wa uongozi baina ya wanasiasa wa eneo la Mlima Kenya vile vile katika chama chake cha Jubilee akiwa kiongozi, yanasemekana kuwa miongoni mwa masuala yaliyomsukuma  kuitisha kikao na viongozi wa eneo hilo Ijumaa.
 
Rais Kenyattta kukutana na viongozi wote wa eneo la Mlima Kenya katika Ikulu ya Sagana kwenye Kaunti ya Nyeri. Zaidi ya viongozi mia nne wa eneo la kati wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo huku ajenda za mkutano huo zikikosa kuwekwa wazi hadi sasa. 
 
Hata hivyo, baadhi ya viongozi waliothibitisha kupata mwaliko huo wamesema kuwa wanatarajia rais Kenyatta atazungumzia kuhusu maendeleo ya eneo la kati na vilevile miradi mbalimbali ambayo haijakamilika. 
 
Aidha inatarajiwa kuwa huenda ushusiano wake na Naibu wa Rais William Ruto vile vile Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga na mjadala kuhusu Ripoti ya Jopo la Upatanisho BBI ukawa miongoni mwa ajenda za mkutano huo
 
Suala jingine ni madai ya baadhi ya viongozi kuwa Rais amepuuza seka muhimu kama vile ile ya majani chai na kahawa inayotogemewa sana na wakazi wa eneo la kati.
 
Mkutano huu unafanyika wakati ambapo Naibu wa Rais William Ruto amesitisha  ziara yake kwenye Kaunti ya Nyeri ambapo alitarajiwa hii leo kuhudhuria hafla ya kuchanga pesa katika Kanisa la AIPCA kwenye eneo la Giakanja.
 
Hii ni mara ya pili naibu Ruto anasitisha ziara yake eneo la Kati ya nchi. Jumapili iliyopita Ruto alilazimika kusitisha kushiriki ibada katika eneo la Gatanga kwenye Kaunti ya Murang'a baada ya rais kutarajiwa kushiriki kanisa katika eneo la Kenol kwenye Kaunti hiyo hiyo na muda mchache  baadaye akifutilia mbali hafla hiyo na badala yake kumtuma waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Fred Mantiang'i .