array(0) { } Radio Maisha | Washtakiwa kwa kuhusishwa na udanganyifu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Washtakiwa kwa kuhusishwa na udanganyifu

Washtakiwa kwa kuhusishwa na udanganyifu

Na Esther Kirong'

NAIROBI, KENYA, Watu wanne miongoni mwao Naibu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Baragoi Kaunti ya Samburu, Simon Situma wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Ijumaa baada ya kukamatwa wakihusishwa na visa vya udanganyifu katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne, KCSE.

Inaarifiwa wanne hao walikuwa wakishirikiana kuwasaidia wanafunzi kushiriki udanganyifu katika Karatasi ya Pili ya Somo la Dini.

Kamanda wa Polisi wa Samburu, Tom Makori amesema wanne hao walikamatwa baada ya polisi kubaini kwamba Naibu Mwalimu Mkuu huyo pamoja na Msimamizi wa KCSE walikuwa wakienda chooni mara kwa mara, naibu huyo akiwashirikisha walimu wawili wa Somo la Dini.

Makori aidha amesema walimu hao wawili walikuwa wamejifungia katika vyoo vya shule hiyo wakitoa majibu na kumkabidhi naibu huyo kuwapelekea watahiniwa kupitia msimamizi wa mtihani huo.

Polisi wanasema safari za naibu huyo kwenda chooni zaidi ya mara nne chini ya dakika arubaini na tano ziliwashangaza hali iliyowalazimu kupiga ripoti kwa Mkuu wa Polisi wa Baragoi aliyewaamuru kumtia mbaroni.

Polisi baadaye walimnasa naibu huyo, walimu wawili na msimamizi huyo huku wakipata vijikaratasi vyenye majibu ya mtihani uliokuwa ukiendelea.

Wanne hao walihojiwa jana katika Idara ya Upelelezi, DCI tawi la Samburu Kaskazini kabla kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Baragoi ambako wamekesha usiku kucha.

Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha, hadi sasa watu thelathini na watano wamekamatwa wakihusishwa na visa vya udanganyifu wa mtihani huo.