array(0) { } Radio Maisha | FKF SI MALI YA KIBINAFSI, HUDUMIA UMA; ADUDA AMUONYA MWENDWA
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

FKF SI MALI YA KIBINAFSI, HUDUMIA UMA; ADUDA AMUONYA MWENDWA

FKF SI MALI YA KIBINAFSI, HUDUMIA UMA; ADUDA AMUONYA MWENDWA

Afisa Mkuu Mtendaji wa klabu ya Gormahia Lordvik Aduda amemwonya Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini FKF Nick Mwendwa.

Akizungumza na dawati la michezo la Redio Maisha mchana alhamisi, Aduda  alionekana mwenye hasira.

“Kabla ya uongozi wake Mwendwa hata ligii kuu nchini KPL ilikuwa bora. Wadhamini walikuwa tena kwa wingi, vilabu vilikuwa bora na wachezaji kwa ujumla walikuwa na maisha yanayo stahili. Lakini baada ya uongozi mpya wa FKF, masaibu yakaanza. Shida kubwa na Nick Mwendwa ni kwamba haambiliki. Ni bwana ambaye ana ubaguzi, mapendeleo na kiburi. Huu ni utoto na ufisadi wa hali ya juu. Kwa ujumla mchezo wa kandanda chini ya uongozi wake umekuwa m’bovu mno. Ukimwona mwambie FKF ni mali ya uma, si ya kibinafsi” Alihamaki Aduda.

Mwaka wa 2016, Shirikisho la FKF lilipata uongozi mpya.  Mwendwa, limbukeni kutoka mitaa ya Kariobangi jijini Nairobi alijitosa katika siasa za kandanda nchini na kurithi mikoba yake Sam Nyamweya.

“Tulikuwa na runinga ya Super Sport na kampuni ya Kenya Breweries wakiwa wadhamini wa ligii kuu nchini. Angalau kila klabu ingepata takriban shilingi laki saba hadi milioni moja kila mwezi. Huu ni mgao ambao ulisaidia pakubwa vilabu ambavyo vinashiriki KPL. Lakini Nick alipoingia uongozini, alitaka ligii kuu iwe na vilabu 18 kutoka kwa 16. Hapo basi mdhamini mkuu Supersport akaamua kutorefusha mkataba na kuondoka nchini. Kugharamia vilabu 16, ni jambo ambalo walikuwa tayari wameshalipangia kwenye bajeti. Nick, aliahidi kugharamia vilabu viwili zaidi, sijui kama KPL washawahi pata mgao wowote kutoka kwa FKF”  aliuliza Aduda kwa ghadhabu huku akiongezea kwamba labda huenda Kenya Breweries  pia walijiondoa kwa sababu hawakuwa na imani na FKF mpya chini yake rais huyo wa FKF.

Mwendwa alionekana kuwa kijana mjasiri mwenye maono ya kuwatoa wakenya Misri hadi Canaan alipo chukua hatamu za uongozi wa FKF. Wengi walikuwa na matarajio makubwa ambayo hadi sasa bado yana ning’inia tu mawinguni huku yakitafuta pa kutua.

Ligii kuu nchini KPL haina mdhamini. Zaidi ya asilimia 70 ya vilabu nchini havina hela vile vile. Timu za taifa Harambee stars na Harambee Starlets huwa na matatizo ya hapa na pale haswa katika maandalizi ya mechi za kimataifa.

Harambee Starlets maajuzi ilivunja kambi ya mazoezi hadi wakati wizara ya michezo ilipoingilia kati. Jumatano, Harambee Stars nao kule Misri karibu wafurushwe hotelini wanapo jiandaa mechi yao ya michuano kufuzu kombe la barani Afrika dhidi ya wenyeji misri, huku maafisa wachache wa timu hiyo wakizuiliwa. Haijulikani hata kama vijana hao wa nyumbani wana mahala popote pa kufanyia mazoezi kabla ya mechi hiyo.

Ikumbukwe pia ni maajuzi tu rais huyo wa FKF alipoikosoa serikali na wizara ya michezo kwa kuishutumu ya kwamba wamezitelekeza timu za taifa kwa ujumla.

Gumzo kubwa sasa ni serikali hiyo ambayo Nick aliikashifu imewatuma wakaguzi wa matumizi ya fedha kukagua jinsi takriban shilingi milioni 244 zilivyo tumika wakati  Harambee Stars ilipo shiriki michuano ya Kombe la Barani Afrika, AFCON mapema mwaka huu.

Kilio hiki cha FKF kuto ajibika si cha Aduda peke yake, lakini wakenya wote washika dau wa mchezo wa kandanda nchini wana haki ya kulalama iwapo hawajaridhishwa. Wakenya wana haki ya kujua mbivu na mbichi. Kati ya wizara ya michezo na FKF, nani analeta mchezo wa danganya toto na kuwapumbaza wakenya

Sasa ni jicho tu, wakenya wanapo subiri mkwaruzano baina na FKF na wizara ya michezo, bado wana matumaini ya kwamba matunda ya mchezo wa kandanda nchini yataliwa siku moja kwa njia ya haki na ukweli.