array(0) { } Radio Maisha | Bunge lataka maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kemikali hatari ya Xylene katika KCSE
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Bunge lataka maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kemikali hatari ya Xylene katika KCSE

Bunge lataka maelezo zaidi kuhusu matumizi ya kemikali hatari ya Xylene katika KCSE

Hatimaye mjadala kuhusu kemikali hatari iliyotumiwa kwa jili mtihani tendaji wa Somo la Kemia na watahiniwa wa kidato cha nne umeingia bungeni huku Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa ikitakiwa kuwasilisha ripoti ya kina kuhusu kilichochangia kutumiwa kwa kemikali hiyo. Kamati hiyo aidha imetakiwa kuwasilisha maelezo kuhusu idadi ya walioathiriwa na kemikali hiyo na hatua zilizochukuliwa kutokana na madhara yake.

Katika kikao cha Bunge la Kitaifa leo hii, Mbunge wa Kilifi Kusini, Ken Chonga ameitaka Kamati ya Elimu ya bunge hilo kuwasilisha ripoti bungeni kueleza idadi ya walioathiriwa na kemikali hiyo akisema visa zaidi vya madhara ya Xylene vinaendelea kuripotiwa miongoni mwa watahiniwa wa kidato cha nne walioitumia katika kufanya mtihani tendaji wa Kemia.

Aidha, bunge linataka maelezo ya ni kwa nini kemikali hatari ya Xylene ilitumiwa na watahiniwa ilhali kuna aina nyingine ya kemikali ambazo zingeweza kutumika. Chonga ameibua madai kwamba uamuzi wa kuitumia kemikali hiyo huenda ulifanywa dakika za mwisho baada ya kubainika kwamba ile iliyostahili kutumika isingetosha.

Hayo yanajiri wakati ambapo shinikizo limeanza kutolewa dhidi ya Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha kujiuzulu kwa kuidhinisha matumizi ya kemikali hiyo hatari katika mitihani. Hapo jana, mtahiniwa mmoja alifariki dunia kwenye Kaunti ya Nakuru na mwingine huko Kisumu kujeruhiwa vibaya baada ya kemikali hiyo kumchoma usoni alipokuwa akiufanya mtihani wa Kemia. 

 Katika Kaunti ya Turkana, walimu wawili na watahiniwa wawili waliathiriwa na kemikali hiyo, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT tawi la Turkana Kenyaman Eriong'oa. Mwalimu wa kike aliye mjamzito aidha alilazwa huko Trans Nzoia, huku wengine wengi wakiwamo wasimamizi wa mitihani vilevile wakilazwa katika hospitali mbalimbali nchini.

Siku chache zilizopita Chama cha Kitaifa cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET kilitishia kuishtaki Wizara ya Elimu na Baraza la Kitaifa la Mitihani, KNEC kwa kutumia kemikali ambazo si salama. KUPPET ilizitaja kemikali za Xylene, Calcium Hypochlorite na Bromine Water kutokuwa salama.

Ikumbukwe tayari Waziri Magoha alikama kuwapo kwa walioathiriwa na kiemikali hiyo, licha ya visa vilivyoripotiwa. Wengi wa Wakenya hasa mitandoani wamemshtumu kwa kukana jambo lililo wazi. Aidha, wanamshtumu kwa uongozi wa kiimla, hali inayowafanya waaathiriwa kuogopa kuzungumzia kwa hofu ya kuchukuliwa hatua na Wizara.