array(0) { } Radio Maisha | Gavana Alex Tolgos ahojiwa kuhusu matumizi ya fedha kwenye kaunti yake
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Gavana Alex Tolgos ahojiwa kuhusu matumizi ya fedha kwenye kaunti yake

Gavana Alex Tolgos ahojiwa kuhusu matumizi ya fedha kwenye kaunti yake

Gavana wa Elgeyo Marakwet, Alex Tolgos amehojiwa kwa zaidi ya saa mbili na maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC mapema leo katika Jengo la Integrity Center jijini Nairobi

Akizungumza na wanahabari baada ya kuhojiwa na makachero wa EACC, Tolgos amesema amehojiwa kuhusu matumizi ya shilingi takribani elfu mia saba na elfu arubaini za ununuzi wa mafuta yaliyotumika kwenye magari ya hospitali zikiwamo ambulensi, kuanzia mwaka wa 2013 hadi mwaka wa 2016 katika kaunti hiyo.

Wakati uo huo, Tolgos amepuuza taarifa za awali kwamba anachunguzwa kuhusu utoaji tenda wa kununua mafuta ya shilingi milioni mia mbili kutoka kwa kituo cha mafuta kinachodaiwa kuwa chake.

<AUDIO>9702

Amesema hana lolote la kuogopa kwani uchunguzi unaondelea ni miongoni mwa majukumu yaliyoptwikwa ofisi ya gavana kufafanua kuhusu matumizi ya fedha katika kaunti.

Awali Tolgos alipuuza madai yanayomkabili kwa kusema yanachochewa na maadui wake wa kisiasa japo leo amesema maswali aliyoulizwa yamehusu jinis fedha zilivyotumika katika idara ya afya.

Mwaka uliopita aliyekuwa Mkaguzi Mkuu Edward Ouko aliibua madai ya ukiukaji wa sheria za ununuzi na utumizi mbaya wa mamlaka katika osifi ya gavana Tolgos hivyo kupendekeza uchunguzi kufanywa ili kuwajibishwa.