array(0) { } Radio Maisha | Oluga taabani kwa kukosa kusitisha mgomo wa madaktari

Oluga taabani kwa kukosa kusitisha mgomo wa madaktari

Oluga taabani kwa kukosa kusitisha mgomo wa madaktari

Mahakama ya Uajiri na Leba imemwagiza Katibu Mkuu wa chama cha Madaktari KMPDU, Ouma Oluga kulipa faini ya shilingi elfu kumi au kufungwa kifungo cha nje cha mwezi mmoja kwa kukiuka sheria za mahakama baada ya kutakiwa kusitisha mgomo wa madaktari katika Kaunti ya Laikipia na Kirinyaga.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu wa Mahakama hiyo - Nzioka wa Makao na ambaye amewakataza wanahabari kufuatilia kesi hiyo ndani ya mahakama amesema Dakt. Ouma alitakiwa kusitisha mgomo huo ambao umechukua muda wa miezi mitano, hali iliyoifanya serikali ya Kaunti ya Laikipia kuiwasilisha kesi hiyo mahakamani.

Mgomo wa madaktari kwenye kaunti hizo mbili unaendelea licha ya Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga, Anne Waiguru na mwenzake wa Laikipia, Nderitu Muriithi kuwafuta wahudumu hao wa afya kwa kushiriki mgomo usiokuwa halali.