array(0) { } Radio Maisha | Wavulana wawili wajiua kwenye Kaunti ya Taita Taveta kwa kujinyonga

Wavulana wawili wajiua kwenye Kaunti ya Taita Taveta kwa kujinyonga

Wavulana wawili wajiua kwenye Kaunti ya Taita Taveta kwa kujinyonga

Polisi katika Kaunti ya Taita Taveta wameanzisha uchunguzi kufuatia visa ambapo wavulana wawili wamejiua kwa kujinyonga kwenye maeneo mawili tofauti.

Katika kisa cha kwanza, mvulana mmoja amepatikana akiwa amejinyonga mapema leo katika kijiji cha Mghange - Saghalla katika eneo la Voi. Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, huenda jamaa huyo alijiua siku tatu zilizopita, kabla ya mwili kupatikana leo.

Katika tukio jingine, mwili wa mvulana mmoja uko katika Hifadhi ya Maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Voi baada ya kujinyonga katika kijiji cha Msisinenyi kwenye eneo la Mwatate.

Visa hivi vinajiri huku viongozi wakitoa wito kwa wakazi kuwashirikisha wandani wao au hata wahubiri wanapokumbwa na matatizo au msongo wa mawazo ili kuepuka hali sawa na hii.