array(0) { } Radio Maisha | Kamati maalum yabuniwa kuchunguza madai ya kuwapo kwa sumu katika mahindi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Kamati maalum yabuniwa kuchunguza madai ya kuwapo kwa sumu katika mahindi

Kamati maalum yabuniwa kuchunguza madai ya kuwapo kwa sumu katika mahindi

Serikali imebuni kamati maalum itakayochunguza madai ya kuwapo kwa sumu kupita kiasi ya aflatoxins kwenye bidhaa hasa za mahindi nchini. Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri na Mwenzake wa Biashara Peter Munya wamesema kwamba wamebuni kamati hiyo  ambayo inawahusisha wataalam mbalimbali  kuchunguza suala hilo.

Munya amesema kwmaba Wizara yake inaendelea kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha kwamba vyakula vinavyouzwa nchini vinaafikia viwango vinavyokubaliwa kwa matumizi ya binadamu.

Kwa upande wake Kiunjuri akihojiwa na Kamati ya Bunge ya Kilimo, ameomba kupewa muda wa wiki mbili ili kukamilisha uchunguzi kabla ya kuwasilisha ripoti yake bungeni.

Wakati uo huo, Bunge la Seneti limeipa hadi Jumatano ijayo Kamati ya Kilimo kuchunguza suala hilo kisha kuwasilisha ripoti yake. Keneth Lusaka ni Spika wa Seneti.

Agizo la Spika Lusaka , linafuatia wito wa baadhi ya maseneta kuitaka serikali kuwachukulia hatua kali maafisa wa Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa Nchini KEBS na wamiliki wa kampuni ambazo bidhaa zake zinadaiwa kuwa na sumu hiyo.

Akiwasilisha hoja hiyo Seneta wa Bungoma Moses Wetangula, amesema hali hiyo inatokana na utepetevu wa KEBS na Bodi ya Kitaifa Nafaka na Mazao NCPB, ambayo anadai ilipuzilia mbali ripoti ya Kamati ya Kilimo ya Bunge.

Kauli ya Wetangula imeungwa mkono na maseneta kadhaa, ambao wamesema ni sharti idara zinazohusika ziwajibike. James Orengo ni Seneta wa Siaya.