array(0) { } Radio Maisha | Chuo Kikuu cha JKUAT chatarajiwa kufunguliwa karibuni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Chuo Kikuu cha JKUAT chatarajiwa kufunguliwa karibuni

Chuo Kikuu cha JKUAT chatarajiwa kufunguliwa karibuni

Huenda Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Sayansi na Teknolojia, JKUAT kikafunguliwa hivi karibuni kufuatia mikutano na washikadau mbalimbali. Amesema Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Victoria Ngumi.

Ngumi amesema wamefanya mikutano na maafisa wa usalama, viongozi wa wanafunzi na baadhi ya wanasiasa ambapo wameafikiana kuwa malalamiko yaliyoibuliwa yatashughulikiwa.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Mbunge wa Gatundu Kusuni, Moses Kuria ambaye amewaonya wafanyabiashara wa dawa za kulevya mjini Juja dhidi ya kuwatumia wanafunzi. Kamishna wa eneo la Kati Wilson Nyagwanga amesema maafisa zaidi wa polisi watatumwa kwenye eneo hilo ili kuimarisha doria.

Wanafunzi wa Chuo hicho waliandamana Jumatatu wiki hii kulalamikia utovu wa usalama na kuulaumu usimamizi wa chuo kwa kutochukua hatua zozote.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Tume ya Huduma za maafisa wa Polisi NPSC kuwataja maafisa watatu miongoni mwa wanne waliohusika na kisa cha kuwachapa wanafunzi wakati wa maandamano hayo. Maafisa hao  George Wathania, Jonathan Kibet na Boniface Muthama, ambao tayari wamesimamishwa kazi kwa muda ili kutoa nafasi ya dhidi yao kufanywa.