array(0) { } Radio Maisha | Serikali yawaonya wanaoendelea kuuza unga hatari
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali yawaonya wanaoendelea kuuza unga hatari

Serikali yawaonya wanaoendelea kuuza unga hatari

Serikali imewaonya wasagaji wa mahindi wa aina tano za unga ambao umehusishwa na kemikali kupita kiasi ya aflatoxin, ambao bado wanaendelea kuuza unga huo licha ya marufuku ya serikali.

Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri, amesema kuwa wizara yake imetambua kuwa baadhi ya wasagaji wa aina hizo tano za unga wamepunguza bei ya bidhaa hiyo ili kuwavutia Wakenya wasiokuwa na ufahamu wa athari yake.

Akiwa mbele ya Kamati ya Kilimo ya Bunge la Kitaifa, Kiunjuiri, amesema kuwa serikali itawakabili wanaotengezea unga uliopigwa marukufu na wamiliki wa maduka kwa hatia ya kupuuza agizo la Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa nchini Kebs. Marufuki hiyo ilitolewa kwa kampuni zinazotengeneza unga wa Dola, Kifaru,  Starehe,  210 na Jembe.

Kebs imesema kuwa utafiti wa Idara yake ya Uchunguzi umebainisha kuwa orodha ya unga kutoka kwa wasagaji hao unakiwango cha juu cha aflatoxin ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu.Kebs aidha amesema kuwa wasagaji wanastahili kusitisha shughuli za kutengeza ungao huo kabla ya leseni zao kupokonywa.

Kiunjuri amesema kuwa serikali inaendeleza msako kwa maduka mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa Wakenya hawaathiriki na matumizi ya unga huo.