array(0) { } Radio Maisha | Watu zaidi waliosimamia shughuli ya sensa walalamikia kutolipwa fedha zao
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu zaidi waliosimamia shughuli ya sensa walalamikia kutolipwa fedha zao

Watu zaidi waliosimamia shughuli ya sensa walalamikia kutolipwa fedha zao

Takriban miezi mitatu baada ya kufanyika kwa shughuli ya kuhesabu watu nchini, baadhi ya maafisa waliosimamia shughuli hiyo kwenye kaunti mbalimbali wanaendelea kulalamikia kutolipwa fedha zao hadi sasa.

Baadhi ya sababu zinazodaiwa kuchangia kutolipwa kwao ni  wengine kupoteza vifaa walivyotumia kwa sensa huku wengine wakiwasilisha nambari za akaunti zenye dosari ambazo walistahili kutumiwa pesa.

Ikiwa ni takriban wiki moja tangu kutolewa kwa matokeo ya idadi ya watu nchini, baadhi ya maafisa walioongoza shughuli hiyo wamelalamikia kutolipwa fedha zao licha ya kujitolea kuhakikisha shughuli hiyo ina faulu. Charles Mogaka ambaye ni mmoja wa waliohesabu watu kwenye Kaunti ya Nyamira, analalamika kwamba hadi sasa hajalipwa shilingi takriban elfu 22 ambazo alinuia kulipwa. Mogaka anasema kwamba sababu ya kutolipwa ni eti alipoteza mojawapo ya vifaa vya alivyotumiwa katika kuhesabu watu..

 

Mwingine mwenye madai sawa na ya Mogaka ni Joseph Musyoka ambaye alishiriki shughuli hiyo kwenye Kaunti ya Makueni.

Tumewasiliana na Susan Marita ambaye alikuwa msimamizi wa shughuli hiyo katika eneo la Bonyaiguba Nyamira na anathibitisha madai ya kutolipwa kwa mmoja wa maafisa aliyowasimamia.

Afisa wa Shirika la Kukadiria Idadi ya Watu kwenye Kaunti ya Nyamira, Jerry Ochieng anakiri kuwapo kwa watu kadhaa ambao hawajalipwa huku akisema kwamba kamati ya kulishughulikia suala hilo itabuniwa ili kuhakikisha malalamishi yaliyoibuliwa yanashughulikiwa.

Je, kilio cha wale ambao hawajapokea malipo kitasikika, ama fedha zao zitapotelea pasipojulikana.