array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa ujambazi auliwa na polisi Kisauni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mshukiwa wa ujambazi auliwa na polisi Kisauni

Mshukiwa wa ujambazi auliwa na polisi Kisauni

Polisi kwenye eneo la Kisauni wamefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi mwanachama mmoja wa genge la vijana ambalo lilikuwa na nia ya kutekeleza uvamizi karibu na Kituo cha Polisi cha Bamburi.

Kamanda wa Polisi kwenye eneo hilo, Julius Kiragu amesema kwamba wamepata taarifa kulihusu genge hilo la vijana kumi ambalo lilikuwa limejihami kwa panga na visu na walipo fika eneo la tukio wakaliamuru kujiwasilisha japo wakakaidi.

Amesema kwamba polisi wamelazika kufyatua risasi kadhaa hewani japo genge hilo likaanza kuwashambulia mafisa hao ndiposa mmoja wao akauliwa huku wengine wakitoroka na majeraha ya risasi.

Polisi wamefanikiwa kupata panga saba na kisu kimoja katika eneo la tukio huku msako dhidi ya wanachama tisa ambao wako mafichoni ukiendelea.

Amesema kwamba mwili wa mwanachama aliyeuliwa umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Rufaa ya Coast General ambako umelazwa japo hajatambuliwa kwani hakuwa na stakabadhi za kumtambulisha.

Amesisitiza kwamba polisi hawatalegeza kamba dhidi ya magenge hayo ambayo yamekuwa tishio kwa wakazi wa Kisauni huku akiwahimiza wanachama kujisalimisha mara moja.