array(0) { } Radio Maisha | Kutuny awataka Rais na Raila Odinga kuweka wazi ripoti ya Jopo la Upatanishi BBI

Kutuny awataka Rais na Raila Odinga kuweka wazi ripoti ya Jopo la Upatanishi BBI

Kutuny awataka Rais na Raila Odinga kuweka wazi ripoti ya Jopo la Upatanishi BBI

Mbunge wa Cherangany Joshua Kutuny amewataka Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga kuweka wazi ripoti ya Jopo la Upatanishi BBI ili kufanikisha maazimio yao ya kutatua migogoro ya kisiasa nchini.

Akihutubu wakati wa hafla ya kumkaribisha Mbunge mteule wa Kibra Imran Okoth katika eneo la DC Grounds, Kutuny amesema Wakenya wana hamu ya kuipokea ripoti hiyo tangu jopo la BBI lilipokamilisha vikao vyake.

Wito wa Kutuny unajiri wakati ambapo tayari washirika wa Naibu wa Rais William Ruto wametishia kuipinga ripoti ya BBI iwapo itapendekeza kuongeza nyadhifa za uongozi serikalini.

Wakati uo huo Imran amewapongeza wakazi wa Kibra na viongozi waliomuunga mkono akiwamo Raila huku akiahidi kutimiza ahadi zake.