array(0) { } Radio Maisha | Polisi wamefanikiwa kulinasa ambalo utumiwa kutekeleza uhalifu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Polisi wamefanikiwa kulinasa ambalo utumiwa kutekeleza uhalifu

Polisi wamefanikiwa kulinasa ambalo utumiwa kutekeleza uhalifu

Polisi wa Trafiki katika eneo la Kisauni Kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kulinasa gari aina ya Toyota ISIS ambalo linakisiwa kutumiwa na magenge ya vijana kutekeleza uhalifu kwenye maeneo kadha ya Mombasa.

Kamanda wa Polisi wa Kisauni Simon Thirikwa amesema kwamba gari hilo lilinaswa leo asubuhi katika kizuizi cha magari katika daraja la Nyali.

Amesema kwamba watu watatu waliokuwa ndani ya gari hilo walitoroka huku mafisa wakifanikiwa kupata panga Tatu moja likiwa na matone ya damu ikikisiwa huenda ilikuwa imetumika kutekeleza uhalifu.


Simu mbili na leseni ya dereva aliyekuwa akiliendesha gari hilo pia zimepatika na zinatumiwa katika uchunguzi. Amesema kwamba tayari mwanamke mmoja amejitokeza kusema kwamba alikuwa amempa mjukuu wake gari hilo bila kufahamu lingetumiwa kutekeleza uhalifu.

Amewashauri wazazi kuwa wangalifu na watoto wao msimu huu wa likizo ili kuwaepusha kujihusisha na masuala potovu.

Polisi wanaendelea kuwatafuta watano hao huku Thirikwa akiwaagiza kujisalimisha mara moja.