array(0) { } Radio Maisha | KWS wamtia mbaron mshukiwa kwa kuuza nyama ya wanyamapori

KWS wamtia mbaron mshukiwa kwa kuuza nyama ya wanyamapori

KWS wamtia mbaron mshukiwa kwa kuuza nyama ya wanyamapori

Maafisa wa Uhifadhi wa Wanyamapori KWS wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja anayedaiwa kuuza nyama ya wanyamapori katika soko la kuuza nyama la Barma.

Martin Njoroge amekamatwa akiwa na nyama inayoaminika kuwa ya pundamilia na nyingine iliyooza ikipatikana katika duka lake.

Maafisa hao wa KWS wamesema wamemkamata mshukiwa huyo baada ya kudokezewa kuhusu shughuli zake katika soko hilo na umma uliomshuku.

Mshukiwa amehamishiwa gereza la Lang'ata kutoka Kituo cha Polisi cha Shauri Moyo alikokuwa akizuiliwa huku akisubiri kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika