array(0) { } Radio Maisha | KEBS, yapiga marufuku matumizi ya aina tano za unga
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

KEBS, yapiga marufuku matumizi ya aina tano za unga

KEBS, yapiga marufuku matumizi ya aina tano za unga

Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa KEBS, limepiga marufuku matumizi ya aina tano za unga wa mahindi unaotumika nchini.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari KEBS imesema aina hizo hazijaafikia viwango vinavyohitajika kwa matumizi ya binadamu.

Unga uliopigwa marufuku ni wa kiwanda cha Dola, Kifaru, Starehe, Two Ten na Jembe.

Kulingana na KEBS ukaguzi uliofanyiwa ulibainisha kuwa unga huo una viwnago vya juu vya sumu aina ya Aflatoxin kuliko vile vinavyokubaliwa.

Wakati uo huo, kampuni za kusaga mahindi zinazouza aina unga huo zimepigw amarufuku dhidi ya kuendelea kutumia nembo ya KEBS, vile vile kuuza bidhaa hizyo hadi pale zitakapoafikia vigenzo vinavyohitajika.

Aidha kampuni hizo zimetakiwa kuondoa unga ambao sasa unauzwa katika soko na maduka ya humu ncini kufuatia marufuku hiyo. KEBS imesema kampuni hizo zitapewa idhini tena baada ya kuhakikisha kuw abidhaa zake ni salama kwa binadamu na baada ya ukaguzi kukamilika tena.

Kampuni zilizoathirika ni Kitui Mills inayosaga unga wa Dola, Alpha Grain Limited inayosaga unga wa Kifaru, Pan African Grain Millers ya Starehe, Kenblest Limited ya Two Ten na Kensalrise ya Jembe.

Wakati uo huo, umma umeshauriwa kuwajibika ili kuhakikisha bidhaa unazotumia ni salama. Ili kubaini iwapo bidhaa hiyo ni salama, KEBS imeshauri kutuma kodi iliyo chini ya nembo ya shirika hilo kwenye bidhaa kwa nambari 20023 ili kupata maelezo zaidi, na iwapo hakuna maelezo unashauriwa kupiga simu kwa nambari 1545 bila malipo.